Hospitali Bubu Yakutwa Nachingwea, Mmliki akiona cha Moto

Na. Ahmad Mmow.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango, jana aliiongoza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kwenda kuvamia na kumkamata mmiliki wa hosipitali bubu iliyopo katika kijiji   cha Mchangani wilayani humu.

Akizungumzia tukio hilo, Muwango alisema alilazimika kwenda mwenyewe pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo baada ya kupata taarifa kwamba hosipitali hiyo imekuwa ikitoa huduma kinyume cha sheria kwa takribani miaka minne bila ya kuchukuliwa hatua zozote. Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kwamba hali aliyoikuta katika eneo hilo haikubaliki. "Mmiliki hana leseni wala kibali kinachomruhusu kutoa matibabu, mwenyewe amekiri kuwa hana leseni wala kibali. Bali afisa tabibu mshahara, anatoa huduma kwa wananchi na anauzoefu" ,alisema Muwango.

Akieleza hali aliyoikuta katika hosipitali hiyo, mkuu huyo wa wilaya alisema mazingira ya kutolea huduma hayafai. Nakuongeza kuwa mmiliki huyo alikuwa anawafanyia upasuaji wagonjwa. Kitendo ambacho ni kinyume na sheria. Alisema licha ya kufanya upasuaji lakini pia walizikuta dawa ambazo haziruhusiwi kuuzwa kwenye maduka ya dawa. "Tulimkuta mgonjwa aliye fanyia upasuaji wa enia kwa malipo ya shilingi 22, 0000. Nimwambia arejeshe fedha hizo kwa mwenyewe na alirudisha.

Mgonjwa huyo alipelekwa hosipitali ya wilaya ambako anaendelea na matibabu. Wagonjwa wanafanyiwa upasuaji juu ya kitanda cha kama, vifaa vinachemshwa kwenye sufuria, "aliongeza kusema Muwango. Alisema dawa na vifaa tiba vilivyokutwa kwenye nyumba hiyo ya makazi ambayo imefanywa kuwa hosipitali vinadhihirisha amekuwa akifanya matibabu ambayo hayalingani na kiwango cha ujuzi alionao.

Kufuatia hali hiyo Muwango ametoa wito kwa wasitahafu waliokuwa wanahudumu serikalini kuzingatia taratibu na sheria wanapoamua kutumia taaluma na ujuzi wao kutoa huduma ili kujiingizia kipato halali. Huku akihaidi kutomuhurumia mtu yeyote ataefanya mambo kinyume cha sheria. Katika kuhakikisha hali hiyo haiendelei katika wilaya hiyo, amewaonya watendaji wa vijiji na kata wasio wafichua watu wanaofanya na kuendesha shuguli kinyume cha sheria katika maeneo yao ya utawala watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa ajira zao.

Huku akimuagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kumchukulia hatua za kinidhamu mtendaji wa kijiji cha Mchangani. "Hao wapo karibu na wanafanya mambo hayo lakini hawachukui hatua, wanasubiri mkuu wa wilaya. wao niwenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama katika maeneo yao lakini hawawajibiki ipasavyo," alisema. Alipoulizwa kaimu mganga mkuu wa hosipitali ya wilaya ya Nachingwea, Dkt Ibrahim Pazia, kuhusu kuwepo kwa hosipitali bubu hiyo na iwapo kuna mgonjwa aliyepelekwa kutoka kwenye hosipitali hiyo, alisema hakuwa katika kituo cha kazi. Yupo safarini.

Juhudi za kumpata kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga hazikuzaa matunda baada ya kutopatikana hewani hadi habari hii inaandikwa. Kwa mujibu wa Muwango mmliki na tabibu huyo aliyemtaja kwa jina la Seleman Martin anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com