Hiki ndicho kilichoandikwa na Zitto na Nay baada ya Roma kutekwa

Kitendo cha rapper Roma Mkatoliki na Moni Central Zone kuchukuliwa usiku wa jana (Jumatano) wakati walipokuwa studio ya Tongwe Records na kupelekwa sehemu isiyojulikana, kimewaumiaza wengi. Zitto Kabwe na Nay wa Mitego ni miongoni mwa walioumizwa na tukio hilo.

Wawili hao wamekilaani kitendo hicho kupitia mitandao tofauti tofauti. “Uvamizi wa studio ya Tongwe na kumkamata msanii Roma Mkatoliki ni mwendelezo wa uongozi wa kigangstar na lazima kulaani Kwa nguvu zetu zote,” ameandika Zitto kwenye Twitter yake.
Naye Nay kupitia mtandao wa Insytagram ameandika, “Kuvamia Ofisi Za watu, heh.! Kumbe nayo ni Kazi.?! Nina Imani uko salama mwanangu, Kamanda @roma2030 Sina ata chembe ya wasi wasi. #Wapo ✊🏿✊🏿.”
Watu hao wanadaiwa kuwachukuwa vijana wengine wawili waliokuwa katika studio hiyo na wameondoka na computer ya studio na Screen (Tv).


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com