Haji Manara atoa kauli hii baada ya kipigo cha jana

Msemaji wa Simba, Haji Manara anaamini kikosi cha Simba kina nafasi ya kubeba ubingwa.

Manara anaamini Simba itabeba ubingwa kama itarekebisha makosa katika mechi tano zilizobaki.

Simba imepoteza mechi mechi yake dhidi ya Kagera Sugar kwa kuchapwa kwa mabao 2-1 wakati ilikuwa na matumaini ya kubaki kileleni hadi mwisho wa ligi.

“Ni kweli tumekosea, ni kweli tumefungwa. Hakuna haja ya kupoteza muda, tuendelee kupambana.

“Bado tuna nafasi, kikubwa tunahitaji utulivu na kurekebisha makosa,” alisema.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com