Gwajima: "Diamond Nimekusamehe ila nikisikia maneno wiki Ijayo Nitafunguka"

Askofu Gwajima leo alikuwa ameahidi kuweka wazi mambo ya Diamond Platnumz kuhusu tetesi zake za kuwa ni Freemason , Lakini amedai kuwa Jana Diamond kupitia mtandao wa Kijamii wa Instagram Alimuomba Msamaha Kwa Mchungaji huyo,

Watu wengi leo walifurika katika kanisa hilo na wengine kutazama live kupitia Youtube wakitarajia kuwa anafunguka makubwa kuhusu Diamond lakini Karibia na Mwisho wa Mahubiri yake alidai Bibilia inasema mtu akiomba Msamaha Hupashwa Kusamehewa hivyo Hata ameamua Kumsamehe na kumsitiri , lakini ametoa onyo kuwa Ajichunge na akisikia maneno maneno wiki ijayo atafunguka....

Gwajima na Diamond wameingia katika vita baada ya Diamond Kumuimba askofu huyo katika wimbo wake uitwao 'Acha nikae Kimya'

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com