Familia ya watu 7 ipo Hoi Hospitali Kwa Kula Mboga zenye Sumu

Watu saba wa familia moja katika kijiji cha Kibuhi wilaya ya Rorya mkoani Mara,wamefikishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara mjini Musoma, kwa ajili ya matibabu,baada ya kula mbona za majani aina ya Mgagani zinazodaiwa kuwa na sumu na kusababisha kupatwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kupoteza fahamu huku baadhi yao warukwa na akili na hivyo kuwafanya kukimbia ovyo.

Baadhi ya ndugu wa wagonjwa hao,wamesema katika hospitali hiyo ya rufaa mkoa wa Mara mjini Musoma kuwa,jioni ya aprili nane mwaka huu,mama mmoja wa familia hiyo,anadaiwa kuchuma mboga hizo katika moja ya shamba kijijini hapo,kisha kuzipika na kula yeye na familia yake kama chakula cha jioni,na kwamba baada ya muda mfupi walianza kujisikia kizunguzungu kabla ya kupatwa na magonjwa hayo.

Muuguzi wa zamu katika hospitali hiyo ya rufaa mkoa wa Mara Bi. Edinnes Makoba,amethibitisha kupokea wagonjwa hao ambao wanadaiwa kula mboga hiyo ya majani aina ya Mgagani.

Chanzo:ITV


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com