Bashe awataka wabunge wa CCM Waache Unafiki.....Kasema Yupo Tayari Kufukuzwa CCM

Mbunge wa Nzega Mjini(CCM) Hussein Bashe amewataka wabunge wa CCM  kuacha unafiki kuhusu kuwateka watu na kwamba yeye ni mmoja wa watu waliokamatwa  na usalama wa taifa wakati wa mkutano Mkuu wa CCM.

"CCM acheni unafiki mimi nimeshakamatwa na watu wa usalama mnasema hawakamati, kwa hili nipo tayari mniondoe kwenye chama". Amesema Bashe

Bashe alikuja juu baada Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene kumtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuthibitisha kuwa matukio ya ukamataji yanafanywa na usalama wa Taifa

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com