Bangi itaanza kuuzwa kwenye maduka ya dawa ifikapo Julai

Nchi ya Uruguay iliyopo Kusini mwa America itakuwa ya kwanza duniani kuuza Bangi kihalali kwa matumizi ya kujiburudisha tu, nchi hiyo ilianza kuhalalisha matumizi ya bangi mnanomo mwaka 2013 baada ya sheria iliyokubali uuzaji na ununuzi wake kupitishwa.
Sheria hii inawataka wanunuzi kujisajili na serikali. Bei yake itakuwa $1.30 kwa gramu moja, Watakaojisajiliwa lazima wawe raia wa Uruguay au wakazi wa kudumu wa nchi hiyo na hawaruhusiwi kununua zaidi ya gramu 40 kwa kipindi cha mwezi mmoja.
“Bangi itauzwa kwenye maduka ya dawa kuanzia Julai,” msaidizi wa Rais, Juan Andre Roballo alisema katika kikao na wanahabari.
Mpaka sasa serikali imeandikisha mkataba na maduka 16 ya kuuza madawa na inatarajia kusajili maduka zaidi.
Roballo amesema kuwa kutakuwa na kampeni ya afya itakayofanywa kabla ya sajili kufunguliwa rasmi.
Alisema kuwa serikali kwa sasa haina uwezo wa kutosheleza mahitaji ya wanunuzi lakini haitarajii idadi yao kuwa kubwa zaidi, kwa sasa marijuana hiyo itakuwa inapandwa kwenye mashamba yanayosimamiwa na serikali.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com