Baba atiwa mikononi mwa polisi kwa kumbaka mtoto wake

Baba mmoja  aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Mademba (39) mkaazi wa Kianga atiwa mikononi mwa polisi kwa kosa la  kumbaka mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka 13.
Taariza zilizothibitishwa na kamanda wa Polisi wa Mjini Magharibi Kamishna msaidizi muandamizi wa Polisi Hassan Nassiri Ali amesema tukio hilo la kusikitisha baina ya mwezi machi na april 19 mwaka huu huko kianga wilaya ya magharibi A.
Aidha kamanda hassan amesikitishwa sana na tukio hilo na kuiomba  jamii  kurudi katika maadili mema kwani ni jambo la ajabu sana kusikia mwana familia kufanya tukio la kinyama katika familia yake.
Hata hivyo amesema Mtuhumiwa wa tukio hilo ameshakamatwa na polisi na baada ya upelelezi kukamilika atapelekwa mahakamni kujibu shtaka lake.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com