Baba amchoma moto bintiye baada ya kugundua kuwa ni 'Mjamzito'

MTU mmoja anaejulikana kwa jina la Mzee Hunge Msholangi anaishi wilayani  Mkalama, mkoani Singida, amejeruhi binti yake kwa kumchoma na moto  baada ya kugundua kuwa binti huyo ni mjamzito.

Mzee huyo anayeishi  kata  ya Ibaga Kijiji cha Ilongo kitongoji cha Ilangida amemjeruhi binti huyo mwenye umri wa miaka 14

Tukio hilo lilitekelezwa Tarehe 21 Aprili  mwaka huu ambapo mzee huyo alianza kumpiga binti huyo  kwa fimbo na baadaye kuchukua  Kuni  yenye moto na kuanza kumuunguza,sehemu za matiti,usoni na inasemekana kaunguzwa sehemu za mapaja

Mama wa mtoto alipotaka kumtetea binti yake   naye alipigwa,na  kuchomwa kwa kuni hiyo yenye moto  shavuni.

Binti huyo alifichwa ndani na baba ,baada ya siku tatu hali ya binti haikuwa nzuri wanafamilia wakaanza kutoa taarifa kwa majirani.

Hatimaye chanzo chetu kinaeleza kuwa  taarifa hizo zikafika kituoni cha polisi Ibaga ,ambapo askari wa jeshi hilo  walifika nyumbani kwa mzee huyo na kushuhudia binti huyo akiwa ndani na hali yake hiyo ya majeraha.

Binti akapelekwa kituo cha afya Makalama  kwa ajili ya matibabu, mpaka sasa mgonjwa yupo Hospitalini hapo huku akiwa hawezi  kuzungumza,JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com