AUDIO ya Bashe: “Kuna watu wamenitumia Meseji kuwa nipo hatarini kufanyiwa Kitu Mbaya"

Mbunge wa Nzega Vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hussein Mohamed Bashe amesema kuwa ametumiwa ujumbe wa vitisho na watu wasiojulikana wakisema kuwa watamfanyika kitu kibaya popote pale alipo.

Bashe ambaye yupo kwenye vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma ameandika leo asubuhi kupitia akaunti yake ya Tiwtter na Instagram  kuwa, ametumiwa ujumbe huo uliosomeka;

“Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale tulipo.

"Bunge na Serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hili la Haramu wakati Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana. "

Kufuatia vitisho hivyo, Mbunge Hussein Bashe amelitaka Bunge na Serikali kutofumbia macho vitendo hivi vya wananchi kutekwa na watu wasiojulikana.

Sikiliza sauti yake Bungeni leo, bonyeza hapa Chini:-


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com