AUDIO: Sakaya amvaa Maalim Seif....Adai yeye Ndiyo tatizo ndani ya CUF

Naibu Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF ambaye pia ni Kaimu katibu Mkuu wa chama hicho Magdalena Sakaya amesema chanzo cha mgogoro unaoendelea katika chama hicho ni katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad

Sakaya ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo ambapo amesema viongozi na wadau mbalimbali wenye mapenzi mema na chama hicho wameshamfuata Maalim Seif ili akutane na Prof Lipumba wamalize tatizo lililopo katika chama hicho lakini Maalim Seif amekataa

Pia amezungumzia suala la uchaguzi wa Bunge la afrika mashariki hususan kwa wagombea wao wa CUF akiwemo Habib Mnyaa na wenzake wawili

Unaweza kumsikiliza zaidi kwa kubonyeza Play hapo chini:-

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com