AUDIO: "Polisi Mkamateni Halima Mdee Mara Moja Kokote aliko" Asema Spika

Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameagiza jeshi la polisi kumkamata Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee popote alipo na afikishwe bungeni

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo Bungeni mjini Dodoma na kusema kuwa Mbunge Halima Mdee akamatwe kutokana na kutumia lugha ya Matusi wakati wa uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki juzi

Pia ameagiza Mh Freeman Mbowe kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni naye akahojiwe kwenye kamati ya Maadili ya bunge kutokana na kutumia lugha mbaya baada ya uchaguzi huo

Msikilize Spika hapa chini akiongela yote hayo kwa kirefu

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com