AUDIO: Maalim Seif kufikishwa Mahakamani kwa Uchochezi, asema IGP Mangu

Jeshi la polisi limesema muda wowote kuanzia sasa litamkamata na kumfikisha mahakamani Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad kwa tuhuma za Uchochezi anaoufanya visiwani Zanzibar

kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Ernest Mangu wakati akihojiwa jana katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Azam

IGP Mangu amesema awali walimruhusu Maalim Seif Kufanya vikao vya ndani kwa nia njema, lakini baadaye wakagundua anavitumia vikao hivyo kuchochea vitendo viovu hasa kwa maasimu wao wa kisiasa

"Baada ya vikao vile ndipo tulipoanza kushuhudia vitendo viovu, Mahasimu wa Maalim Seif wakichomewa moto mikarafuu yao, Tulimuita na tulimhoji, jalada lake lipo kwaa DPP na muda wowote kuanzia sasa Tutamfikisha mahakamani" amesema IGP Mangu

Unaweza kumsikiliza kwa kubonyeza Play hapa Chini:-


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com