Abdi Banda wa Simba aomba radhi mashabiki

Mchezaji wa klabu ya Simba, Abdi Banda ameomba radhi kwa mashabiki wa soka nchini kwa kitendo chake cha kumpiga ngumi, kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla Jumapili katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Banda alikuwa na bahati tu kwa kutopewa kadi nyekundu baada ya kumtwanga ngumi Kavilla katika mchezo ambao Simba ilifungwa 2-1.
Baada ya siku mbili Banda ameamua kuvunja ukimya na kuomba radhi kwa kitendo chake hicho.
“Nachukua nafasi hii kuwaomba radhi Watanzania na kaka yangu (Kavilla) kwa tukio lilitokea Jumapili, kwa sababu mimi na yeye ndiyo tunajua kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea,”amesema Banda.
Banda amesema kwamba alikutana na Kavilla baada ya mchezo kumuomba radhi ana kwa ana kwa kitendo kile, lakini ameona haitoshi bali pia awaombe radhi wapenzi wa soka kupitia vyombo vya Habari.
Source: binzubeiry


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com