Wezi waiba mtambo wa ATM

Tumezoea kusikia wezi wakivamia Benki na kuchukua fedha, lakini hii iliyotokea Nairobi Kenya ni ya tofauti kutokana na njia iliyotumiwa na wezi kuiba mtambo wa ATM ukiwa na fedha ndani yake.
Kutokana na tukio hilo jeshi la polisi Nairobi Kenya limemkamata mlinzi wa Benki ya Equity akihusishwa na wizi huo ambao ulitokea mwishoni mwa wiki.
Wezi hao walitoweka na kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana mpaka sasa, unaambiwa wezi walichimba ukuta wa nyuma wa Benki hiyo na kutoweka na sanduku la kuhifadhi pesa pamoja na mtambo wa ATM, pesa zikiwa ndani. Washukiwa hao waliweza kuzima kamera za CCTV na pia kengele ya usalama kabla ya kufanya tukio hilo la wizi.
Akizungumza na BBC, kamanda wa jimbo la Nairobi Japheth Koome amesema kwamba polisi waliweza kupata mitungi ya gesi na vifaa vingine ambavyo hutumika kukata chuma.
Source: BBC

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com