Wananchi wazuia Mkutano wa CCM Mkoani Morogoro

Mkutano wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Morogoro umesimama kwa muda baada ya wananchi wa tarafa ya Mvuha wilaya ya Morogoro kuandamana wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali kwa madai yakupinga hatua ya baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo kuhamisha makao makuu kutoka kijiji cha Mvuha kuelekea kijiji cha Lundi kinyume na maagizo yaliyowahi kutolewa na viongozi wakuu wa serikali.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha ITV kimeshuhudia wananchi hao wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali mbele ya mkuu wa wilaya hiyo Bi, Regina Chonjo na mbunge wa jimbo la Morogoro kusini Prospa Mbena ambapo wakizungumza kwa jaziba wananchi hao wameiomba serikali kuu kuingilia kati sintofaham hiyo ambayo inaweza kuleta uvunjifu wa amani kwa wananchi hao.

Akizungumza mbele ya wananchi hao mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi Regina Chonjo amewaomba wananchi hao kuwa watulivu huku akisisitiza msimamo wa serikali wa kuhamisha makao makuu ya halmashauri hiyo kutoka mjini Morogoro kwenda tarafa ya Mvuha kama ambavyo imekuwa ikielekezwa na viongozi wakuu wa serikali katika awamu zilizopita. 


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com