Wananchi waleta Vurugu Tanga, Wafunga Barabara

Vurugu kubwa zimetokea katika kijiji cha Mabalanga wilayani Kilindi mkoa wa Tanga baada ya wanakijiji hao kufunga barabara wakishinikiza serikali kushughulikia mgogoro uliopo kati ya kijiji hicho na kijiji cha Mafuleta mgogoro ambao umechukua muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi na vilevile wametaka viongozi wao waliokamatwa kwa kuhusiana na mgogoro huo kuachiwa na wao ndipo watafungua barabara.

Vurugu hizo ambazo zimedumu kwa takribani masaa saba kuanzia saa tisa arasili hadi saa mbili usiku baada ya wananchi hao kufungua barabara hiyo wamesema kuwa wamefanya hivyo kwa kuishinikiza serikali kuachia viongozi wa kijiji hicho waliokamatwa kwa madai kuwa wamekuwa vichochezi wa mgogoro huo.

Ufungaji wa barabara hiyo ambao ulizuia zaidi ya magari 40 na abiria wapatao 150 kukwama kuendelea na safari zao baadhi ya abiria wamesema kuwa serikali ishughulikie mgogoro huo kwa haraka. 

Mwandishi wa habari hii alimtafuta mkuu wa wilaya ya Kilindi Bi Sauda Mtondoo kwa njia ya simu na kukiri kutokea kwa hali hiyo na kuwataka wananchi kutochukua sheria mkononi. 

Hali hiyo ilimalizika saa mbili na nusu usiku baada ya viongozi hao kuachiwa na ndipo wananchi wakafungua barabara na abiria kuendelea na safari zao.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com