Wananchi Wachukua maamuzi Magumu, Wajenga Madaraja ya Miti Mto Idigima

Wananchi wa vijiji vya Shasya na Lwati katika kata ya Harungu wilayani Mbozi mkoani Songwe wameanza kujenga madaraja ya miti katika mto Idigima unaotenganisha vijiji hivyo kwa kutumia nguvu zao ili kuondoka na kero ya zaidi ya miaka 35 ya kuvuka mto huo unapofurika pamoja na kuwezesha watoto wanaosoma shule za msingi na sekondari zilizo ng’abo ya mto huo kwenda shuleni nyakati za masika.

Uamuzi wa wananchi kujenga madaraja ya miti kwenye mto Idigima unatokana madhara waliyokwishayapata wakati wa kuvuka mto huo ikiwemo vifo nyakati za masika na hasa wanafunzi wanapokwenda shuleni ng’ambo ya mto huo.

Jitihada za ujenzi wa madaraja hayo tayari zimeungwa mkono na diwani wa kata ya Harungu, Maarifa Mwashitete pamoja na mbunge wa jimbo la Mbozi, Pascal Haonga Wamabo wametumia mfuko wa jimbo kuwezesha upatikanaji zana za ujenzi kama vile saruji, hali ambayo imewafanya wenyeviti wa vijiji vya Shasya na Lwati kuiomba serikali nayo kuunga mkono jitihada za wananchi hao kwa kujenga barabara hiyo angalao kwa kiwango cha changalawe ili iweze kupitika mwaka mzima.

Diwani wa kata ya Harungu, Maarifa Mwashitete amesema mto huo umekuwa kero kwa wananchi tangu mwaka 1979 na kwamba wao kama viongozi wameamua kuonyesha njia ya kuondokana na kero hiyo.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com