Wachina wakamatwa wakiiba maji Mkoani Dodoma

Wakazi wa mtaa wa Area A manispaa ya Dodoma wamekosa huduma ya maji kwa zaidi ya wiki tatu baada ya kampuni ya Selcom kutoka uchina inayojenga mitaro ya barabarani katika eneo hilo kukata kwa makusudi mabomba ya maji na kujiunganishia kinyemela kwa ajili ya matumizi ya ujenzi bila kufuata utaratibu.

Wakizungumza baada ya maofisa wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mjini Dodoma DUWASA kwa kushirikiana na jeshi la polisi kuvamia eneo la ujenzi la wakandarasi hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema wakazi hao wanadai tangu kuanza kwa ujenzi huo wamekosa huduma ya maji hali iliyowasababishia usumbufu mkubwa na kuongeza gharama za maisha.

Ester Galinoma ni kaimu afisa mapato wa DUWASA ambaye anasema kitendo kilichofanywa na wakandarasi hao kimeisababishia mamlaka hiyo hasara kubwa na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma akiwataka wananchi kuwa mabalozi wazuri kwa kuwafichua wezi wa maji ili huduma hiyo iboreshwe mjini Dodoma.

Kwa upande wake msimamizi wa ujenzi katika eneo hilo raia wa uchina hakuweza kutoa ufafanuzi wowote kuhusu tukio hilo kutokana na kutofahamu lugha ya kiswahili wala kingereza.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com