Waathirika Wa Tetemeko Kagera waombwa Kujijengea Wenyewe

quakeSerikali imewaomba wakazi wa Mkoani Kagera waliothirika na tetemeko la ardhi kuendelea kujijengea wenyewe kwani michango yote ya thamani ya bilioni 5.4 iliyochangwa na wadau kwa ajili ya kusaidia walioathirika imeelekezwa kwa taasisi za serikali siyo wanachi binafsi.
Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Mstaafu Salum Kijuu amesema kuwa hadi sasa wadau wamechanga jumla ya bilioni 5 na milioni 427, na kati ya hizo bilioni 1 na milioni 130 zimekwisha tumika katika kukarabati miundombinu ya serikali iliyoathirika, na kwamba fedha zilizobaki bilioni 4 na milioni 296 nazo zimeelekezwa huko.
Aidha amewatoa wasiwasi wananchi kwamba waathrika wanaosubiri kupata msaada binafsi watalazimika kusubiri michango itakayotolewa na wadau wengine, waliohaidi kusaidia waathrika moja kwa moja, na kwamba hata misaada hiyo ikipatikana watasaidia waathirika walio katika makundi maalum kama wazee na walemavu.
Wakati huo Kampuni ya kuzalisha saruji ya Simba Cement imetoa msaada wa mifuko elfu 1 ya saruji kwa walioathirika wa tetemeko hilo, na saruji hiyo imekabidhiwa kwa mkuu wa Mkoa wa Kagera na Ofisa masoko wa kampuni ya Simba Bw Lesilie Masawe.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com