Vigogo Hatari wa Pembe za Ndovu Wafikishwa Mahakamani

Watu sita akiwemo  Yusuph Ali Yusumbu marufu kama Mpemba wamefikishwa  katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka manne ya uhujumu uchumi baada ya kututwa na pembe za ndovu zenye thamani ya zaidi ya shilingi  milioni 783.

Washtakiwa hao  wamefikishwa mbele ya hakimu mkazi  Thomas Simba  na kusomewa  mashtaka hayo na mwendesha mashataka  wa serikali Paul  Kaduchi. Kaduchi  aliambia mahakama kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa manne ambapo kwa nyakati na sehemu tofauti katika  mikoa ya  Dar es Salaama, Morogoro, Iringa, Tanga  na Mtwara  wakiwa na mtu mwingine ambaye hayupo mahakamni hapo  walikutwa na pembe za ndovu  mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika shtaka la kwanza  mwendesha mashtaka huyo alisema kati ya January 2014 na October 2016 washtakiwa hao  walikutwa na  pambe za Ndovu  50 vyenye thamani ya shilingi milioni 392,817,600  na kuongeza kuwa katika shtaka la pili  October 26 mwaka  huu  huko Mbagala, Zakhem  jijini Dar es Salaam  walikutwa na zenye uzito kilogramu 13.85 venye thamni ya shilingi  milioni 65,469,600.

Mahakama ikaendelea kuambiwa kuwa shtaka la tatu October 27 mwaka huu  huko Tabata Kisukulu  washtakiwa hao  walikutwa na kilo 11.1 zenye thamani ya shilingi  milioni 32,734,800. Na katika shtaka la mwisho mahakama imeambiwa kuwa  October 29 mwaka huu huko Tabata Kisukulu Ilala jijini Dar es Salaam  washtakiwa hao walikutwa na vipande 36 vya pembe  za Ndovu  vyenye thamani ya uzito wa gramu 58.55 vyenye thamani ya shilingi milioni 294,613,200.

Hata hivyo washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kisheria kusikilisha mashauri hayo na hivyo kesi hiyo itatajwa tena Desemba moja mwaka huu.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com