Urambo ni vilio tu baada ya kuuaga mwili wa Samuel Sitta


NIWAMLILIA SIMANZI KILA KONA URAMBO,  SITTA

Mamia ya wananchi mkoani Tabora wamejitokeza kumuaga kipenzi chao Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel Sitta aliyefariki usiku wa kuamkia Jumatatu ya wiki hii.

Wananchi hao wamejitokeza katika Uwanja Shule ya Msingi Urambo jirani ya nyumbani kwake Sitta. Shughuli ya kutoa heshima za mwisho wa wananchi hao imeanza saa moja asubuhi.

Wananchi hao walijipanga katika mstari mrefu kwa ajili ya kupita pembeni mwa jeneza lenye mwili wa Sitta, ambapo toka asubuhi maduka mengi wilayani Urambo yalikuwa yamefungwa.

PICHA NA EDWIN MJWAHUZI

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com