Unyama: Wazazi Wamcharanga Vibaya Mtoto Wao Mchanga Usoni!

KATIKA hali isiyo ya kawaida, wazazi wa mtoto mmoja mchanga wamecharanga usoni mtoto huyo kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kumsababishia maumivu makali na kuvuja damu nyingi.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni katika Mji wa Kwara nchini Nigeria ambapo wazazi hao (majina yao hayakufahamika) wamedai kuwa kumfanyia hivyo mtoto mchanga ni sehemu ya kutimiza mira na desturi za utamaduni wa kabila lao. Aidha walieleza kuwa watamjulisha kilichotokea kuhusu kuchanjwa kwake siku za mbele akiwa mtu mzima.

tribal-mark-1
Aidha wanaaini kuwa, alama hiyo ya kikabila ni kafara ambayo inatambulisha urembo aliyonao Mwafrika. Ni sehemu ya utamaduni wa watu waishio Kusini Magharibi mwa nchi ya Nigeria, Kaskazini mwa Nigeria na Kusini Mashariki mwa Nigeria.
zxxx3858
Wao humwandika mtoto sehemu za mwili wake kwa kumuunguza na moto au kwa kucharanga wakati mtoto akiwa mchanga ikiwa ni alama ya kutambulisha kabila, familia au jamii inayotumia urithi wa mfumo dume (patrilineal ).
Kazi nyingine ya alama hiyo ni ishara ya urembo na ubunifu ambayo hufanywa zaidi na watu wa Nigeria, Kenya, Benin, na Togo.
Tamaduni za kuwekwa alama kwa watoto wachanga zilianza wakati wa biashara ya watumwa ambapo baadhi ya watumwa wa jamii moja waliungana kwa kutambuana kupitia alama hizo, hivyo ikawarahisishia kujenga misingi ya umoja na kudai haki zao ikiwemo uhuru.
Tamaduni hizo kwa sasa zinaonekana kupitwa na wakati hivyo watu wameanza kuzipiga vita wakitaka zifutwe kwani zinakiuka haki za binadamu kwani husababisha maumivu makali kwa watoto wakati wa kuchanjwa, kuvuja damu nyingi na wakati mwingine kupelekea vifo.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com