Timbwiri Kesi ya Godbless Lema na Mkewe Neema

Na Mwandishi Wetu
KUTOKA jijini Arusha, Kesi ya kumtukana RC wa Arusha Mrisho Gambo, inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mh Godbless Lema na mke wake Neema Lema, imeshindwa kusikilizwa maelezo ya awali. Hatua hiyo ni baada ya Mbunge huyo kukwama kuletwa Mahakamani toka Mahabusu kwa sababu zisizojulikana.

Ikumbukwe Ijumaa iliyopita Lema alipelekwa Gereza la Kisongo, Arusha baada ya kunyimwa dhamana katika kesi nyingine ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, hatua ambayo imepingwa na chama chake na mawakili wake. Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Calist Lazaro alisema hawakuridhishwa na pingamizi la dhamana lililowekwa na mawakili wa Serikali kwani tayari Lema alikuwa amepewa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi siku hiyo ya Ijumaa.

Lakini kwa matarajio ya wengi leo walikuwa na imani ya kumuona Mbunge huyo kwenye viunga vywa Mahakama kwa muendelezo wa kesi yake na mambo ya dhamana, lakini Mbunge huyo hakuonekana Mahakamani, ambapo kulimradhimu Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Agustino Rwezile kutoa amri ya kutolewa hati ya kumtoa Mahabusu mshitakiwa huyo na kumleta mahakamani hapo ili kesi hiyo isikilizwe maelezo ya awali.
Mpaka saa saba mchana Mbunge huyo hakuletwa kwenye viunga vywa Mahakama, kwasababu zisizofahamika, ingawa kulikuwa na amri ya Hakimu iliyotolewa saa nne asubuhi, licha ya mke wake kuwepo mahakamani hapo. Hakimu Rwezile alimtaka wakili wa serikali kueleza sababu za kushindwa kumleta Lema Mahakamani wakati Mahakama imetoa amri.

Wakili wa serikali Fotunatus Mhalila alisema mshitakiwa ameshindwa kuletwa Mahakamani kutokana na sababu zisizozuilika , ila kwa sababu upelelezi umekamilika aliomba Mahakama ipange tarehe ya usikilizaji wa hoja za awali.

Majibu hayo yalipingwa vikali na Wakili wa utetezi, John Mallya ambaye alitaka kufahamu sababu za kutomleta Lema anazodai hazikuweza kuzuilika ni zipi na kwa nini zisitajwe  mahakamani. Baada ya hoja hizo kutolewa Hakimu Rwezile aliendelea kusisitiza hati ya kumtoa Mahabusu itolewe ili aletwe Mahakamani leo katika kesi hiyo, ambayo itasikilizwa hoja za awali.

Awali katika kesi hiyo Godbless Lema na mke wake Neema, alisomewa mahitaka kuwa kati ya Agosti 20 Mwaka huu ndani ya Arusha, walimtumia ujumbe wa simu ya kiganjani RC wa Arusha wenye lugha ya matusi , huku wakijua ni kosa kisheria.Ilidaiwa kuwa ujumbe huo ulitumwa kutoka namba mbili za voda kwenda namba ya RC huyo ya Voda ukidai, “Karibu, tutakuthibiti kama Uarabuni Wanavyothibiti Mashoga.”


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com