Shule ya Nyasi Mkoani Ruvuma Yaibua makubwa, Wanafunzi wanapishana na Tembo Njiani

Wanafunzi wa shule ya msingi miembeni iliyoko katika kijiji cha Likuyu-Mandela wilayani  Namtumbo mkoani Ruvuma wanasomea kwenye shule iliyoezekwa kwa nyasi huku shule hiyo yenye wanafunzi 230  wa awali hadi darasa la pili inafundishwa na mwalimu mmoja ambapo  wanafunzi wa darasa la tatu hadi la  saba wakisafiri umbali mrefu kwenda shule nyingine ambako njiani hupishana na tembo.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Miembeni mwalimu Theodore Ngatunga amesema kuwa  anatembea  umbali mrefu kwenda shuleni hapo njiani akipishana na tembo kwa kuwa kijiji  cha Likuyumandela  kina tembo wengi wanaotokea kwenye pori la Selou huku wanafunzi nao wa darasa la tatu hadi la saba wakipishana na tembo njiani hivyo ameiomba serikali kujenga shule yenye hadhi na nyumba za walimu.


Kwa upande wao  wake mwenyekiti wa shule hiyo bw. Mijai Kacheche   ambayo pia  ina uhaba wa madawati ambapo wanafunzi huandika wakiwa wamekaa chini huku wa awali,darasa la kwanza hadi la pili wakisomea kwenye darasa moja  anasema kuwa  wamefyatua tofali zaidi ya laki moja za kujenga shule yenye hadhi lakini uwezo wa kuendeleza ujenzi hawana.

Akizungumza kwa njia ya simu  mkuu wa wilaya ya Namtumbo Bi. Lacknes Amlima amesema kuwa wilaya hiyo ina shule za nyasi nyingi na shule hiyo ni miongoni mwake na kwamba  upo mpango wa kufyatua tofali na kujenga shule  zenye hadhi  na kuachana na shule hizo za nyasi.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com