RC Makonda ataka Kuwe na eneo moja la Kuzika Viongozi, Atamani Nyerere afukuliwe azikwe Dodoma

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kutengwa sehemu maalumu kwaajili ya kuwazika viongozi mbalimbali waliofanya mambo muhimu katika nchi.
watsap-cover-1848
Makonda ametoa ombi hilo wakati akizungumza katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam katika shughuli za kuagwa marehemu Samuel Sitta.
“Na ombi langu mheshimiwa rais ninalolileta kwako, ikiwezekana kama kutakuwa na nafasi tunao viongozi wengi sana akiwepo Baba wa Taifa Mwalimu Kambarage Nyerere, wakina Molinge Sokoine siku zinavyokwenda unafikia wakati historia zao zinapotea. Hili ni ombi ambalo nalileta mbele ya mwili wa Baba yetu. Tulikubali makao makuu ya nchi yetu yawe Dodoma tuwe na eneo maalum na mahususi kwaajili ya kutenga na kuwahifadhi na kuwazika viongozi wetu waliofanya jambo kubwa katika historia ya maisha yetu ili iwe kumbukumbu kwa kizazi na kizazi kitakwenda na kusoma historia zao na kujua nini walifanya katika taifa letu,” alisema Makonda.
“Kama Ufaransa, yapo makaburi ya viongozi na wananchi waliofanya makubwa ambayo yamebaki kama sehemu ya kumbukumbu. Kwahiyo nilikuwa naomba pale Dodoma tutenge ardhi sehemu ambayo itabaki kama kumbukumbu ya kuwahifadhi viongozi wetu na Mungu ikimpendeza tutaubeba mwili wa mpendwa wetu Mwalimu Julius Kambarage nyerere kuuleta Dodoma kama sehemu ya watu kujifunza historia ya nchi yetu,”ameongeza


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com