Polisi wakamata Waganga wa Jadi Matapeli Makambako Njombe

JESHI la polisi mkoa wa Njombe  linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kufanya shughuli za uganga wa jadi bila kuwa na kibali na kubandika matangazo ya shughuli zao katika mji wa Makambako na kusababisha watu kutapeliwa.

Kamanda Protas amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika wilaya ya kipolisi Makambako ambako ndio walikuwa wakifanyia shughuri zao na kukutwa na vitu mbalimbali vya kufanyia shughuli a kiganga kama mkia wa ngombe, pembe, vibuyu na mashine za kuchapishia matangazo hayo.

Amesema kuwa watuhumiwa hao wamewakamata wakiwa na mabango ambayo yapo tayari kwa kubandikwa mitaana yakiwa na namba zao za simu.

Hata hivyo amesema kuwa uchunguzi bado unaendelea na kuwa ukikamilika watawafikisha mahakamani huku akitoa wito kwa jamii kuwa makini na mabango yanayobandikwa mitaani.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com