Picha 16 za ajali ya basi la Mwafrika Igosi Njombe

Basi la Kampuni ya Mwafrika Safari lenye namba za usajili T 252 BPA linalofanya safari zake Makete hadi Iringa limepinduka katika kijiji cha Igosi wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe

Kwa mujibu wa mashuhuda wanasema chanzo cha ajali hiyo ni kuchomoka kwa tairi la mbele la upande wa kulia hali iliyopelekea dereva kushindwa kulimudu na kupinduka

Ajali hiyo imetokea jana mchana na haikufahamika mara moja kama kumetokea vifo wala idadi ya majeruhi, na basi lililopata ajali lilikuwa likitoka Iringa kuelekea Makete

Taarifa zaidi tutakujulisha tukizipata, na hapa chini kuna picha za ajali hiyo

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com