Nyumbani Kwa Samwel Sitta Ni Vilio Tu

Waombolezaji na viongozi mbalimbali wameendelea kujitokeza kutoa salam za pole kwa familia ya aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samweli Sitta aliyefariki ujerumani juzi kwa Maradhi ya Tezi Dume.

Viongozi walio wasili nyumbani kwa Marehemu mtaa wa Rufiji Masaki jijini Dar es salaam leo ni pamoja na Mzee Waziri wa Afya wa Zamani Profesa Philemon Sarungi, Mbunge wa zamani wa Kahama Mhe. James Lembeli, Mbunge wa zamani wa Mafia Mhe Abdul Karim Shah, Mbunge wa zamani wa Songea na Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi pamoja na Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mhe. Mwantumu Mahiza .

Msemaji wa familia, Bw. Gerlad Mongella amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili Dar es salaam siku ya Alhamisi majira ya saa nane na kupelekwa nyumbani. Siku ya ujumaa mwili wa marehemu utaagwa kuanzia majira ya saa tatu hadi saa sita katika viwanja vya Karimjee, kabla ya kuelekea mkoani Dodoma kwa ajili kuagwa rasmi na waheshimiwa wabunge.

Bw. Mongella amesema kuwa ratiba ikienda kama wanavyotarajia, mazishi ya kiongozi huyo yatafanyika siku ya Jumamosi huko nyumbani kwake Urambo mkoani Tabora.

Amesema wanafamilia wanashukuru ndugu jamaa na marafiki  kwa kuendelea kwao kufika hapo nyumbani na kuwafariji katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

 mmoja wa waombolezaji akiwa ameinama kwa uchungu baada ya kusaini  katika daftari la maombolezo nyumbani kwa Marehemu mtaa wa Rufiji Masaki jijini Dar es salaam leo


Waziri wa zamani Profesa Philemon Sarungi akitoa mpole kwa mtoto wa Marehemu,Agnes Sitta katika msiba wa aliykuwa spika wa zamani Samuel Sitta.

 Dkt Emmanuel Nchimbi akisaini kitabu cha Maombolezo 
 Wabunge wastaafu wakiwa kwenye maombolezo ya Marehemu Samwel Sitta
Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Banji,akimpa pole Meya wa Kinondoni Benjamini Sitta. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. paul Makonda. Picha zote na Humphrey Shao wa Globu ya Jamii.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com