News Alert: Mwanamke anaswa na Meno ya Tembo Chumbani MwakeJeshi la polisi mkoani Simiyu limemkamata mwanamke mmoja akiwa na pembe za ndovu zenye uzito wa kilo 32 akiwa amezificha chini ya uvungu wa kitanda chake.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu Kamishina Msaidizi Mwandamizi Onesmo Lyanga amesema Novemba 13, mwaka huu majira ya saa 9:30 Alasiri katika kijiji cha Ipililo wilayani Maswa,askari wa kitengo cha intelijensia walipata taarifa na kufika nyumbani kwa mtuhumiwa na walipompekua nyumbani kwake wakaweza kukamata meno mawili ya tembo yaliyokuwa yamefichwa uvunguni.

Chanzo: ITV

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com