Mwalimu abaka mwanafunzi wake Huko Kagera

Jeshi la polisi mkoani Kagera limefanikiwa kumkamata Azaria Kareshu ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi ya Kakindo iliyoko wilayani Muleba mkoani Kagera na kumfikishwa mahakamani ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 14 ambaye jina lake limehifadhiwa.

Mwalimu huyo amefikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Muleba Cleophace Wanne na amesomewa mashtaka yanayomkabili na mwendesha mashitaka wa Jeshi la polisi Charles Mpewa,mwendesha mashtaka huyo amesema mshtakiwa anatuhumiwa kutenda kosa hilo Septemba 10,mwaka huu katika kijiji cha Magatta kilichoko wilayani Muleba,mshtakiwa pamoja na kupata dhamana hakutakiwa kujibu lolote hadi upelelezi wa kesi hiyo utakapokamilika,kesi hiyo itatajwa tena Novemba 25,mwaka huu.

Kufuatia tukio hilo,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba, Emmanuel Sherembi amemsimamisha kazi kwa muda mwalimu Azaria Kareshu anayekabiliwa na tuhuma ya kumbaka mwanafunzi ili apishe uchunguzi wa tuhuma inayomkabili pia ametoa onyo kwa walimu wanaoenda kinyume na maadili ya taaluma hiyo. 


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com