Mnyika aibuka, Alazimika kumpigia magoti Rais Magufuli

BAADA ya Wakazi wa Mbezi na Kibamba kubomolewa nyumba zao Mbunge wa jimbo la Kibamba John Mnyika wa Chama Cha  Demokrasia na Maendeleo [Chadema] ameibuka na kumuomba Rais John Magufuli, kuingilia kati na kukumbuka makubaliano waliyofikia wakati akiwa Waziri wa Ujenzi.

Mnyika, alisema ikumbukwe  wakati huo akiwa Mbunge wa Ubungo aliwasilisha maelezo binafsi bungeni juu ya Wakala wa Barabara (Tanroads) walipotaka kuendesha operesheni ya bomoa bomoa katika maeneo hayo.


Spika Makinda aliponiita kuyasoma nililijulisha Bunge kwamba tayari kuna makubaliano na Waziri wa Ujenzi wa wakati huo Magufuli kwamba kazi hiyo isifanyike kutokana na makubaliano hayo,"

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mnyika alisema inasikitisha kuona wananchi wakiishi kama wakimbizi baada ya kubomolewa nyumba zao.

Alisema lengo la hoja yake hiyo ilikuwa ni kuwanusuru wananchi hao kwa kuzingatia makubaliano hayo, lakini alishangaa kuona serikali ya awamu ya tano ikiendesha operesheni ya bomoabomoa kila kona tena bila huruma.

Mnyika, amesema serikali imekuwa ikibomoa nyumba za wananchi wake bila huruma huku ikijua fika kwamba hadi wananchi hao wanajenga katika maeneo hayo, makosa hayakupata vibali yametoka kwa maofisa wa serikali,"alsema Mnyika.

Alisema Rais asipokuwa na huruma na wananchi ipo haja ya serikali kufunguliwa kesi ya kukazia hukumu ya wananchi wa Mbezi ambayo iliwapa wananchi haki pamoja na wananchi wa maeneo mengine ya Kibamba nao kufungua kesi.

Hivi karibuni wakazi wa Mbezi na Kibamba wamekumbwa na bomoabomoa ambayo imeziacha baadhi ya familia zikiishi katika mazingira magumu.

Wananchi hao walidai kuwa operesheni hiyo ilienseshwa bila ya kuzingatia sheria kwani wakati inaanzishwa baadhi ya wananchi hawakupewa taarifa rasmi ambapo nyumba zao zilikuwa hazimo katika mpango wa kubomolewa, jazikuwa na alama ya X.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com