Mkuu wa wilaya amwamuru Mkurugenzi kuwasimamisha kazi watumishi watatu

Na Rhoda Ezekiel globu ya Jamii,Kigoma,

MKUU wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma Luice Bura amemtaka  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo kuwasimamisha kazi watumishi watatu katika kitengo cha ujenzi kwa tuhumaa za ubadhirifu wa fedha kiasi cha Sh.Milioni 109 kati ya sh.milioni 264 zilizotakiwa kumaliza mradi wa vyumba vitatu vya madarasa na nyumba ya walimu yenye uwezo wa kuishi familia za watu sita na matundu matano ya vyoo katika Sekondari ya Itaba katani humo.

Maagizo hayo aliyatoa Jana katika kikao cha ulinzi Na usalama ambacho yeye ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo baada ya kufika eneo la Ujenzi wa vyumba vya madarasa Na vyoo katika shule za sekondar tank Na Nyumba za walimu Na kukuta vyoo havija sakafiwa Na vyumba vingine havijajengwa.

Bura aliwataja watumishi watakao simamishwa ni pamoja na Salehe Mbogoye, Felix Ngomano na Haruni Mbapaye kutoka idara ya ujenzi , ambao ndio waliokuwa wakisimamia ujenzi wa majengo hayo na kuchangia upotevu wa sh.milioni 109, ilihali kiasi cha sh.milioni 46 zimelipwa bila kufanyiwa kazi na ujenzi uliofanyika upo chini ya kiwango huku ujenzi upo chini ya asilimia 50% na kuidhinisha malipo hewa

" baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kutokana na mradi huo niliamua kuituma Kamati ya ulinzi na usalama ,walifika katika eneo la ujenzi na kukuta ujenzi haujakamilika ambapo matundu ya choo ni mashimo tu, madirisha hayapo sakafu haijawekwa na ninakuomba Mkurugenzi uwasimamishe kwa muda watumishi hao hadI uchunguzi utakapo kamilika kutokana Na tuhuma hizo",alisema Bura.

Hata hivyo Bura alisema cha kushangaza Madiwani wa kamati ya ujenzi waliomba posho ya kufanya ukaguzi wa ujenzi na wakapewa posho ya siku tano ,kumbe hata kwenye eneo la ujenzi hawajafika hali iliyowapelekea watumishi wengine kuangukiwa na barua za maadili ni pamoja na Ofisa Elimu Sekondari Wilaya Honolata Kabundugulu, Fedy Eliasafu Ofisa Maliasili na Ofisa kilimo wilaya Said Shemahonge ambao wataitajika kujibu tuhuma hizo. 

Akitoa ufafanuzi juu ya mradi huo Mjumbe wa kamati ya maendeleo ya kata husika Bosco Ngomagi alisema serikali ihakikishe inashirikisha wananchi wa eneno husika,ili kuondoa uhujumu uchumi wa jamii ambapo kamati husika watasimamia mradi husika Na wannchi wtafuatilia kwa ukaribu ilikujua no kiasi gani kimetengwa ilikuweza kukamilisha mradi Na mradi ukamilike kwa wakati.

Nao baadhi yaVibarua kutoka kampuni iliyochukua zabuni ya ujenzi ya Mangalazi Engenearing ya Kigoma Mjini Paschal Leonardi walimuomba mkuu huyo awasaidie malipo yao kwa kuwa fedha nyingi zimeshatumika Na wao hawajapata malipomyao mpakasasa wanaendelea Na kazi lakini mpakaka sasa kunabaadhi wamechukua fedha hizo bado hawajawalipa.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com