Mchungaji amlamba vibao mwandishi wa habari Kanisani Kwake

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Emmanuel Majora ameripotiwa kumchapa vibao mwandishi wa habari wa Star TV, Theodora Mrema katika vurugu zilizotokea kanisani.

Vurugu hizo zilitokana na mvutano wa kupinga ndoa iliyokuwa inafungwa kanisani hapo zikianzishwa na mwanamke mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mke halali wa bwana harusi, Ngarame Neema

Mwanamke huyo aliyekuwa na wenzake alipinga kufungwa kwa ndoa hiyo, hali iliyosababisha fujo kubwa na maharusi kukimbia kila mmoja kusikojulikana. Jeshi la polisi liliingilia kati na kuwakamata wanawake hao.

Akizungumzia mkasa wa kupigwa vibao na mchungaji huyo, Mrema alisema kuwa alikuwa akichukua picha za video wakati wa vurugu iliyokuwa ikiendelea, ndipo mchungaji huyo alipomshika kichwa kwa nguvu kumzuia kabla ya kumchapa vibao vya nguvu.

“Nilikuwa napiga picha wanawake wakipakizwa kwenye gari la polisi, ghafla alikuja Mchungaji na kunikamata kichwani kwa nguvu kisha kunizaba vibao huku wengine wakinishambulia,” Theodory anakaririwa na Mtanzania.

Hata hivyo, baada ya Jeshi la Polisi kuzima vurugu hizo na baadhi ya watu kurejea kanisani, mchungaji huyo alimuomba msamahama Mrema kwa kitendo alichomfanyia.
“Naomba unisamehe, zilikuwa ni hasira tu, sisi sote ni Wakristo,” Mchungaji huyo alimueleza Mrema.

Baada ya yote vurugu hizo kumalizika na wanawake walioanzisha kushikiliwa na Jeshi la Polisi, maharusi walirejea kanisani na ndoa ikafungwa kama ilivyokuwa imepangwa.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com