Makubwa: Polisi akamatwa akimfanyia mtihani Mwanafunzi wa Kidato cha Nne

Jeshi la Polisi Zanzibar limemfukuza kazi askari wake baada ya kukamatwa akimfanyia mtihani mwanafunzi wa kidato cha nne kinyume na sheria huku kukiwa na taarifa za baadhi ya wanafunzi kukamatwa kwa kuhusika na kukutwa na mitihani ya kidato cha nne.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa mjini Magharibi kamishna msaidizi mwandamizi SACP Hassan Nassir amethibitisha kwa jeshi la polisi kumfukuza kazi askari huyo F9592 Hassan Haji Jecha ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa chuo kikuu akichuka digrii ya pili amekutwa  akimfanyia mtihani mwanafunzi Said Haji kitendo ambacho ni aibu.

Katika hatua nyengine blog hii iliwakuta wazee waliojazana nje ya makao makuu ya polisi mkoa wa mjini Magharibi wakilalamika watoto wao kuwekwa ndani bila ya taarifa kwa madai ya kuvujisha mitihani ya kidato cha nne kupitia mitandao ya simu wakiongea nasi baadhi ya wazee wa watoto hoa wameshangazwa na uamuzi wa polisi kutoa taarifa yeyote wanafunzi hao idadi yao haijajulikana wamekamatwa kutoka sehemu mbalimbali huku pakiwa na taarifa ya baadhi ya wataalam kutoka Dar es Salaam wamewasili Zanzibar kufuatia suala hilo.

Hata hivyo wakati wazee hao wanawalilia watoto wao wakiwa ndani ya jengo la polisi kamanda Hassan Nassiri amepinga madai hayo akidai hana taarifa za kuwepo kwa tatizo hilo la kukamatwa wanafunzi kwa shtuma za mitihani hiyo ya kidato cha nne.

Chanzo: ITV


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com