Makamu wa Rais apanda Bombadier, Aelezea Ilivyo Nzuri na ya Uhakika


Serikali ya awamu ya tano imeendelea na hatua yake ya kupunguza matumizi baada ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kusafiri na msafara wake kwa ndege ya ATCL.

Safari hiyo ambayo ilihusisha maofisa 16 wa Serikali  imegharimu Sh7.6 milioni badala ya Sh40 milioni ambazo zingetumika kukodi ndege.

Akizungumza kabla ya kupanda ndege hiyo, Samia alisema ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha huduma za ATCL.

"Nimeamua kusafiri na ndege hii pamoja na msafara wangu huu ili kuunga mkono juhudi za Serikali yetu kwa ATCL, pia uzalendo na kupunguza gharama za matumizi hapa tungesafiri kwa ndege ya kukodi tungetumia takribani Sh40 milioni," alisema.

Samia alipanda ndege hiyo saa 9 jioni  alitarajiwa kuwasili Mwanza saa 10.20 jioni.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com