Lema apewa Dhamana, baadaye mahakama yaifuta

Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema ambaye alishtakiwa kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya viongozi wa serikali, leo November 11.2016  amefikishwa mahakamani ambapo hata hivyo amenyimwa dhamana kutokana na sababu mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Arusha zinaeleza kuwa, katika kesi hiyo leo watu mbalimbali walifurika kwa wingi  nje ya Mahakama hiyo  huku ulinzi mkali ukiimalishwa ndani na nje ya viunga vya Mahakama hiyo.
Taarifa zinaeleza kuwa, Lema amenyimwa dhama kwa sababu  ya Usalama wa Rais na wake mwenyewe  hata hivyo baada ya dakika kadhaa kurejea kwa Hakimu, na kuamuru dhamana aliyoruhusu itenguliwe mpaka hapo itakapoamuliwa vingine.
Lema amerejeshwa tena  mahabusu mpaka hapo kessi hiyo itakapotajwa tena.
Taarifa zaidi zitawajia punde.
Mbunge wa Arusha Mh. Godbless Lema akiwapungia mikono wafuasi wake wakati wa kutoka nje ya Mahakama Arusha akirejea Mahabusu leo Novemba 11.2016 
Ulinzi ukiwa umeimalishwa nje ya Mahakama hiyo
15002503_10211736101984351_3535954325709352430_oBasi la Magereza likiondoka Mahakamani hapo
Baadhi ya wananchi waliofurika kwa wingi kushuhudia kesi hiyo


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com