Lema akosa dhamana, arudishwa mahabusu mpaka Novemba 22


Harakati za kumpatia dhamana mbunge wa Arusha Mh Godbless Lema anayekabiliwa na kesi ya uchochezi zimeendelea kugonga ukuta baada mahakama kuu kanda ya Arusha kusikiliza hoja za pande zote na kuahidi kuzitolea uamuzi baada ya siku tano.

Hatua hiyo imekuja baada ya mawakili wa pande zote kuwasilisha hoja zao kila upande ukitetea hoja yake mbele ya jaji wa mahakama hiyo Mh Sekela Moshi.

Jopo la mawakili wanaomtetea Mh Lema wakiongozwa na wakili msomi Peter Kibatala, John Malya, Adamu Jabiri, Sheki Mfinanga na Charles  Adirian Faraji Mangula walimweleza Mh jaji Sekela Moshi kuwa taratibu za kuweka pingamizi zilikiukwa hivyo shauri hilo litupiliwe  mbali na mteja wao apewe dhamana. 

Kwa upande wa mawakili wa serikali walioongozwa na wakili msomi Paul Kadushi na Moses Marandu nao waliendelea kushikilia na kutetea hoja yao kuwa mtuhumiwa hastahili kupewa dhamana kwa sababu ambazo walishaziwasilisha na kwamba pingamizi waliloweka linakubalika kisheria na kama mtuhumiwa anaona kuwa lina mapungufu anapashwa kukata rufaa na sio kuwasilisha barua kama alivyofanya.

Baada ya mvutano wa mjadala mkali wa kisheria wa mawakili hao wa pande mbili Mh jaji Sekela Moshi akaiambia mahakama kuwa kulingana na uzito wa hoja anahitaji muda wa kuzipitia na kwamba atatoa maamuzi siku ya jumanne tarehe 22 .11.2016.

Kufuatia maamuzi hayo mtuhumiwa Lema alirudishwa tena mahabusu kusubiri siku ya tarehe 21.11.2016 atakapopandishwa kizimbani tena kuendelea na kesi yake ya msingi ya uchochezi na maneno ya kashfa  kwa viongozi wa serikali na pia siku ya tarehe 22 /11/2016 atakapofikishwa mahakamani hapo kujua hatma yake ya dhamana.

Wakati wote kesi ilipokuwa inaendelea ulinzi uliimarishwa ndani na nje ya mahakama na wote waliochele walikatazwa kuingia wakati kesi inaendelea wakiwemo viongozi waandammizi wa Chadema kutoka  makao makuu walioongozwa na mjumbe wa halmashauri kuu vijana taifa Joseph Kasambala.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com