Kesi ya Scorpion yakamilika, Kuanza Kusikilizwa Novemba 30

Upelelezi
wa kesi ya kudaiwa kumtoboa macho, kumjeruhi tumboni na kumpora fedha na mkufu Said Mrisho inayomkabili mkazi wa Machimbo Yombo jijini Dar es Salaam, Salum Njwele (34) maarufu kama Scorpion umekamilika na kesi inatarajiwa kuanza kusikilizwa Novemba 30, mwaka huu.

Hayo yamesemwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo  na Hakimu Flora Lymo anayesikiliza kesi hiyo.

Wakati wa kesi hiyo, mtuhumiwa Scorpion aliomba asomewe maelezo ya awali lakini hakimu Lymo alikataa.

Scorpion anadaiwa kutenda makosa hayo Septemba 6, mwaka huu eneo la Buguruni Sheli wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo anatuhumiwa kuiba mkufu rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34 ukiwa na thamani ya Sh 60,000, bangili na fedha taslimu Sh 331,000 vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh 476,000 mali ya Mrisho.

Wakati wa kusikilizwa kesi hiyo iliyovuta hisia nyingi za watu hususani wakazi wa jijini Dar ulinzi ulikuwa mkali muda wote.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com