Ishu ya Kilimo cha Chai Njombe

Wakulima wa zao la Chai katika tarafa ya Lupembe mkoani Njombe wametakiwa kuungana na kuwa na misimamo ya pamoja ili kunusuru bei ya zao hilo ambayo inaonekana kutowanufaisha kwa muda mrefu licha ya uwepo wa viwanda viwili vya kusaga majani mabichi ya Chai katika maeneo yao. 

Wamesema kuwa kinachopelekea bei ya zao hilo kutowanufaisha ni wawekezaji kuwapangia bei ambapo kwa sasa wangali wanauza majani mabichi ya Chai kwa shilingi 250 kwa bei ambayo haikidhi gharama za uzaliushaji.

Katika mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha ushirika cha LUPEMBE AMCOS Baadhi ya wananchama wameonekana kuitupia lawama bodi ya chama hicho kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ikiwemo kutofanya mikutano ya mwaka kwa muda mrefu. 

Kaimu mrajisi wa ushirika ambaye ni afisa ushirika wa mkoa wa Njombe Exaudi Sapali amewaambia wanachama hao kuwa kutokana na kuwa na mashamba makubwa ya Chai wanaweza kujenga kiwanda chao na kukiendesha ili kuondokana na hasara wanayoipata. 

Chama cha ushirika Lupembe Amkosi kinawanachama zaidi ya 400 na kinamtazamo wa kuanzisha kiwanda chake pamoja na kuandaa mashamba kupanda miti ya mbao na chai.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com