Inasikitisha: Polisi ajiua kwa kujipiga Risasi, Angalia Picha Zake Hapa


Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, aliyetambulika kwa jina la PC Sengerama amefariki dunia baada ya kudaiwa kujipiga risasi ya moto kifuani jana majira ya alfajiri wilayani Tandahimba mkoani humo.
Inadaiwa kuwa wakati askari huyo anafanya hivyo alikuwa katika lindo kwenye Benki ya NMB, Tandahimba.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Henry Mwambambe amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema bado hawajafahamu chanzo cha askari huyo kujiua.
“Ni kweli kama mlivyosikia, askari huyo amefariki dunia alfajiri ya leo (jana) kwa kujipiga risasi, lakini bado hatujafahamu nini chanzo cha kujiua.
“Jeshi la Polisi linaendelea uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo, taarifa zikipatikana zenye ufasaha tutawaambia,” amesema Kamanda Mwambambe.
Taarifa zingine zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa, mwili wa marehemu umesafirishwa jana hiyo hiyo kupelekwa nyumbani kwao mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com