Hatari: Angalia jinsi wezi wa LUKU walivyokamatwa

Shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Ilala limeendelea kuwanasa wananchi wanaotumia Umeme bila kulipa kwa kuwatumia mafundi bandia maarufu Vishoka kuzichezea mita za Luku ili kuwezesha mteja kutumia umeme bila kulipia…
Katika zoezi lililofanyika Jana nyumba moja iliyopo eneo la Upanga namba 238 imebainika kuwa mita yake ilichezewa ambapo ilikuwa ikipitisha Umeme na kutumika huku mita hiyo ikiwa imezimwa.
Katika eneo la kariakoo jengo moja na ghorofa mita tatu za Luku zimeonyesha kuchezewa huku wakazi wake wakiendelea kutumia Umeme bila kulipia kinyume cha sheria ambapo mmoja wa wapangaji amejitetea kuwa kudai kuwa hakujuwa kama mita yake imechezewa.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com