Habari Nzito: CCM Yatuhumiwa Kuuza Shule Dar

Na. Fredy, M
DAR ES SALAAM – Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inatuhumiwa kuuza Shule ya Sekondari ya Tegeta, iliyipo Tegeta wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam, ikiwa na umiliki halali wa Jumuiya hiyo, inadaiwa kuuzwa kinyemela kwa Chuo Kikuu cha Mzumbe cha mkoani Morogoro.
Kwa mujibu wa Tovuti ya Zamampya imebaini shule hiyo itatumika na Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa matumizi ya Kampasi yao ya Dar es salaam, taarifa za kuuzwa kwa shule hiyo yenye kidato cha kwanza hadi cha sita, imeleta hofu kwa wanafunzi wa kidato cha sita wanaotarajia kufanya mitihani ya kitaifa mwakani na kulete sintofahamu kwao.
Ingawa uongozi wa Jumuiya umesema watawapelekwa shule nyingine kwa ajili ya kuendelea na masomo yao, huku wanafunzi wa kidato cha nne wakiwa wanamalizia mitihani ya kitaifa (NECTA) na mwanafunzi wa kidato cha pili wakianza mitihani yao ya kitaifa, wakati kitado cha kwanza, tatu na tano wakisubiri kufanya mitihani ya kumaliza muhura wa pili kwa mwaka 2016 bila kujua hatima yao mwakani.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo alisema shule hiyo haijauzwa kama watu wanavyodai, bali imefidiwa na Chuo cha Mzumbe kwa baraka za Baraza la Wadhamini la Jumuiya hiyo kwa hofu ya kushindwa kujiendesha baadaye kutoka na changamoto ya sera ya elimu bure huku wakiendelea kumiliki shule zaidi ya 60 nchini.


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com