Beki Kisiki wa Azam FC aikimbia Timu Hiyo na Kusaini Timu Mpya

Baada ya kushushwa hadi kikosi cha pili katika klabu ya Azam FC beki  kisiki na raia wa Ivory Coast,Serge Wawa amerejea katika klabu yake ya zamani ya El Merreikh na kusaini miaka miwili utakaomuweka hadi 2018.

Wawa raia wa Ivory Coast alijiunga na Azam FC akitokea katika klabu hiyo ya Sudan na alikuwa waziri wa ulinzi katika timu hiyo na kuisaidia kutwaa kombe la klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati pamoja na Ngao ya Jamii.

Lakini amerejea tena Sudan ikiwa ni siku chache baada ya kueleza kuwa Kocha Zeben Hernandez ambaye anainoa Azam FC kuonyesha kuwa hana mpango naye hii imekuja baada ya kuwa kwenye majeruhi ya muda mrefu.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com