AUDIO:Wananchi wa Ndulamo Makete Wauza Msitu wa Kijiji Wawakomeshe "Mafisadi wa Maji" Kijijini hapo

 Mradi wa maji wanaodai wananchi hao kuwa ulichakachuliwa kwa kuwekewa mabomba feki


 Mambomba yaliyofukiwa yakivujisha maji ilihali ni mapya
 Mwenyekiti wa kijiji cha Ndulamo Bw Tweve akiongoza mkutano huo na wananchi
Kutokana na tatizo la maji linalokikabili kijiji cha Ndulamo kata ya Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe, uongozi wa kijiji hicho umelazimika kuitisha mkutano wa dharura wa kuipatia ufumbuzi kero hiyo ya maji

Katika mkutano huo wa dharura ulioitishwa jana kijijini hapo wananchi hao wamelazimika kukubali kuuzwa kwa sehemu ya msitu wa kijiji uliopo jirani na zahanati ya kijiji chao ili fedha zitatazopatikana zitumike kununulia mabomba ili kuondoa tatizo hilo la maji

Baadhi ya wananchi waliozungumza mkutanoni hapo wamepewa nafasi ya kutoa maoni yao kabla ya kutoka na maazimio ya pamoja ambapo wamesema wamechoshwa na tatizo hilo ambalo linakaribia kufikia mwaka mmoja lakini wakiendelea kuteseka kutembea umbali mrefu kufuata maji mtoni na kwenye vidimbwi

Katika mkutano huo Afisa mtendaji wa kijiji hicho Majuto Mbwilo akatolea ufafanuzi zaidi wa suala hilo la maji kijijini hapo kwa kueleza sababu zilizopelekea tatizo hilo kuwepo kuwa ni mradi wa TASAF wa miaka iliyopita (2013) kuwapelekea mabomba yaliyopo chini ya kiwango ambayo kwa sasa yamepasuka na yanavujisha maji na kila yanapokarabatiwa hasa kwenye viungo bado yanaendelea kupasuka


Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Lilio Tweve ndiye aliyeongoza mkutano huo na baada ya majadiliano ya muda mrefu na wananchi, wakakubaliana kuuza kwa mnada msitu wa kijiji hicho Jumamosi ya wiki hii na fedha zitakazopatikana zielekezwe kwenye kumaliza kero hiyo ya maji, na akatangaza maazimio ya mkutano huo kuhusu maji mbele ya waanchi wote

Unaweza kusikiliza sauti za Mkutano huo kwa kubofya hapa chini


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com