AUDIO: Wazazi wenye watoto waliohitimu Darasa la 7 Ndulamo Makete Wapewa Amri

Wananchi wa kijiji cha Ndulamo kata ya Iwawa wilayani Makete, wamekumbushwa kuhakikisha watoto wao wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani, wanaripoti shuleni kama sheria zinavyotaka

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bw. Majuto Mbwilo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji hicho kuhusu utekelezaji wa agizo hilo la serikali

Bw Majuto amesema wapo wazazi wengine wameshawatafutia shughuli watoto hao huko mijini jambo ambalo ni kinyume na sheria na kuwataka wazazi hao wawaandae watoto hao kwa ajili ya kuanza masomo ya sekondari Januari mwakani kwani elimu ya sekondari ni lazima na sio hiari

Katika hatua nyingine Afisa mtendaji huyo amewaonya wanafunzi ambao wanatarajiwa kuanza kidato cha kwanza mwakani wenye lengo la kutohitimu kidato cha nne kuwa waache fikra hizo, kwa kuwa nao kuhitimu kidato cha nne ni lazima isipokuwa kwa sababu zisizoepukika ikiwemo kifo, huku pia akitoa onyo kwa wazazi wanaoshirikiana na watoto wao kuhakikisha hawaendelei na masomo


Sikiliza sauti hapo chini:-


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com