AUDIO: Wananchi Makete Wazua Kasheshe kwenye Mkutano, Kisa Uzazi wa Mpango

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji cha Ndulamo wilayani Makete mkoani Njombe hasa wanawake wamefurahia elimu ya uzazi wa mpango iliyotolewa katika mkutano wa dharura wa kijiji hicho uliokuwa na lengo la kujadili kero ya maji kijijini hapo kutokana na suala hilo kuonekana gumu tangu miaka iliyotangulia huku wanaume wakiendelea kulipinga suala hilo

Wananchi hao wakiongozwa na wanawake waliokuwa wakishangilia mara kwa mara wamefurahia huduma hiyo itakayotolewa Novemba 19 katika zahanati ya kijiji hicho bila malipo yeyote

Akitoa elimu hiyo Mwakilishi kutoka Marie Stoppers Makao makuu Dar es Salaam Bw Omari Magana amesema huduma zitakazotolewa ni kufunga kizazi kwa wale waliotosheka na watoto, kuweka kipandikizi, kitanzi, na huduma zote zitatolewa bure

"Kina baba mlioko hapa naomba niwaambieni kitu, mimi hapa mnavyoniona hapa mbele yenu nimefunga kizazi na suala hili haliathiri maisha yako ya kila siku, mimi tayari nimeshazaa watoto wangu ninaohitaji na ndio maana nimefunga" amesema Omari huku akichekwa na wananchi hao

Bw Omari amesema baba bora katika familia amekuwa akipanga uzazi kwa kushirikiana na mke wake kwa lengo la kupata familia iliyobora, huku akiwashauri wanawake ambao wameonekana kuumizwa na suala la uzazi na kuwataka kusimama imara kulitetea suala hilo

Wakizungumza kuhusu hilo bila kutaja majina yao Baada ya kuruhusu maswali, baadhi ya wananchi wameelekeza lawama zao kwa kina mama kuwa wengi wao wamekuwa wakienda kufunga kizazi au kutumia njia za uzazi wa mpango kimya kimya bila kuwashirikisha waume zao, huku wengine wakifunga ilihali bado baba anahitaji kuzaa watoto wengine


Sikiliza sauti ya tukio hilo hapa chini:-


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com