AUDIO: Wananchi Ilindiwe Makete watembea zaidi ya Kilomita 20 kupata Matibabu

Diwani wa kata ya Mang'oto Mh Osmundi Idawa akihojiwa na mwandishi wa habari hii.

Kutembea umbali wa kilomita zaidi ya 20 kufuata huduma za afya katika zahanati ya Mang'oto kwa wananchi wa kijiji cha Ilindiwe kata ya Mang'oto wilayani Makete mkoani Njombe ni la kawaida kwao licha ya kuwa na zahanati ya kijiji iliyokamilika ujenzi wake miaka 3 iliyopita.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii mwenyekiti wa kijiji  cha Ilindiwe Bw.Josephati Polepole amesema zahanati hiyo imeanza kujengwa mwaka 2012 na imekamilika mwaka 2014 ambapo mpaka sasa bado haijaaanza kutumika na kwamba zaidi ya shingili milioni 35 zimetumika kujenga zahanati hiyo.

Osmundi Idawa ni diwani wa kata ya Mang'oto anakiri kuwa wananchi wa kijiji cha Ilindiwe wanapata shida ya kusafiri umbali wa kilomita 20 kufuata huduma katika zahanati ya kijiji cha Mang'oto.

Akizungumza suala hilo kwa njia ya simu Mganga Mkuu wa wilaya ya Makete Dkt.Joseph Gaspar Kimaro amesema kinachochelewesha kupeleka watumishi katika zahanati hiyo ni suala la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma linaloendelea nchini kote hivi sasa.

Ameongeza kuwa changamoto nyingine kwa sasa wanasubiri mgawo wa dawa ili ziweze kupelekwa kijiji hapo ambapo wamewataka wananchi wa kijiji hicho kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF ili kupata mgao wa dawa kutoka bohari ya dawa MSD.

Na Henrick Idawa
Sikiliza sauti hizi hapa chini:-


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com