AUDIO: Amri ya Kutumia Stendi Mpya ya Tandala Makete Yapamba moto


Katika kuhakikisha stendi mpya ya Tandala katika wilaya ya Makete mkoani Njombe inaendelea kutumiwa na vyombo vya usafiri pongezi zimetolewa kwa wamiliki wa vyomo vya usafiri hususan Mabasi ya abiria kwa kuanza kuitumia stendi hiyo.

Akizungumza nasi Mwenyekiti wa kijiji cha Tandala Bw Andowisye Memba ametoa pongezi hizo kwa kusema kuwa ushirikiano wanaoutoa ni mzuri na kuwataka wasafiri kutambua kuwa kwa sasa stendi iliyopo katika kitongoji cha Singida, ndiyo inayotambulika rasmi na inaendelea kufanya kazi.
Aidha amewatoa wasiwasi abiria watakaoshukia katika stendi hiyo Kwa kusema kuwa watapata usafiri mwingine wa pikipiki hivyo waendelee kuitumia stendi hiyo.

Pia ameongeza kuwa kwa sasa hawatatumia kituo kingine kushusha  abiria mbali na stendi mpya ya Tandala.

na Asukile Mwalwembe
sikiliza sauti hapo chini kwa kubofya play

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com