Angalia Lema alivyotinga mahakamani na biblia mkononi

Wakati Lema akipelekwa mahabusu kusubiri Hatima ya dhamana yake siku ya Ijumaa tarehe 11 November 2016 baada ya kusomewa mashitaka ya uchochezi  ameondoka akiwa na Bibilia ambayo maadiko yote yapo katika Bibilia  Takatifu
;;;;;;

Mbunge wa Arusha Mh Godbles Lema amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Arusha na kusomewa shitaka la uchochezi na maneno ya kashfa dhidi ya viongozi wa serikali akiwemo Mh Rais Dk.John Magufuli na kisha kupelekwa gerezani baada ya kunyimwa dhamana.

Baada ya mh lema kufikishwa katika mahakama hiyo chini ya ulinzi mkali  mh  Lema alisomewa shtaka la kosa hilo analodaiwa kulitenda katika maeneo  mbalimbali na kwa nyakati tofauti mbele ya hakimu Mfawidhi wa mahakama  hiyo  Desder Kamugisha.

Akiwa mahakamani hapo wakili wa serikali mwendesha mashtaka wa serikali  aliiambia Mahakama hiyo kuwa Mh Lema alitenda kosa hilo tarehe 22/10 2016 Mh Lema akiwa katika eneo la kambi ya fisi kata ya Ngarenaro,kosa ambalo  pia alilirudia katika mikutano mingine ukiwemo uliofanyika  katika kata  ya Baraa.

Baada ya kusomewa shtaka hilo Mh Lema alikana na ndipo ukafika muda wa  mawakili wake kuomba dhamana ambayo hata hivyo ilikataliwa na upande wa  walalamikaji ambao ni wakili wa seikali kwa madai kwamba Mh Lema awali alikuwa na kesi nyingine mbili katika Mahakama hiyo na alipopewa dhamana alifanya tena makosa kwa nyakati tofauti.

Hali hiyo iliibua mvutano wa mawakili wa pande zote,huku mawakili wa  upande wa Lema ulioongozwa wakili John Malya lakini hadi mwisho Hakimu  Mfawidhi wa Mahakama hiyo Desderi Kamugisha alikubali ombi la wakili  wa  serikali la kukataa dhamana na kudai kuwa anataka apate muda wa  kujiridhisha na akaahidi kuwa atatoa uamuzi kukubali ama kuendelea kukataa  dhamana siku ya Ijumaa tarehe 11/11/2016.

Baada ya maamuzi hayo Mh Lema alipandishwa kwenye Karandinga na kupelekwa  magereza tukio ambalo liliibua hali ya taharuki kwa baadhi ya wafuasi  wake waliokuwa mahakamani hapo ambao hawakutarajia huku wakili wake John Malya  akisema kuwa watasubiri kuona maamuzi yatakayotolewa  siku hiyo ya Ijumaa.

Hii ni mara ya pili kwa Mbunge huyo wa Jimbo la Arusha Mh Godbless Lema  kupelekwa magereza katika kipindi chake cha miaka sita ya ubunge huku  akiwa ameshakamatwa na kuhojiwa na kufikishwa mahakamani mara kadhaa kutokana na madai ya makosa mbalimbali ya kisiasa .


JIUNGE NA eddy blog SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Eddy Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com